Product Description
Kitabu hiki cha pekee ni mkusanyiko wa mahubiri ya kusisimua yanayochochea matumaini, faraja na ukuaji kiroho kwa kila mtu--mkubwa na mdogo. Hotuba za pekee zilizobadilisha maisha ya watu wengi Afrika na Amerika Kaskazini zimejengwa katika Biblia, Agano Jipya. Msomaji anapozisoma atapata muonjo wa kile ambacho kiliwafanya maelfu ya watu waliomsikiliza Mchungaji Christopher Mwashinga akihubiri wafurike kumsikiliza. Ni matumaini yetu kwamba msomaji atapata uzoefu mpya kabisa asomapo mahubiri haya na kufurahia utamu wa Neno la Mungu liwaongozao wanadamu katika kumjua Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo aliyemtuma (Yoh. 17:3).